TANZANIA KUWA KITOVU CHA TIBA UTALII VERTEX TUMEJIPANGA KUTOA HUDUMA BORA

Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu amesema kuwa Tanzania inakwenda kuwa kitovu cha Tiba Utalii kwa kutoa huduma za Afya kwa wagonjwa maalumu wa ndani na nje ya nje. Waziri Ummy aliyasema hayo alipofungua mradi wa kliniki mpya ya wagonjwa maalum na wa kimataifa iliyopo katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) itakayotoa huduma za kliniki kwa wagonjwa wa ndani na nje ya nchi.

“Haya tutakayoyashuhudia leo ni matokeo ya uwekezaji mkubwa ambao Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan amefanya katika Sekta ya Afya lakini pia niwapongeze Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI) chini ya Prof. Abel Makubi na Mwenyekiti wa Bodi Prof. Charles Mkony kwa kazi nzuri na kubwa ya kuokoa maisha ya Watanzania”. Amesema Waziri Ummy.

Waziri Ummy amewaomba Watanzania wenye uhitaji wa tiba kwa haraka (kliniki ya wagonjwa maalum na Wakimataifa) ikiwa ni mtumishi au mfanyabiashara waende MOI ambapo ndani ya masaa mawili unamaliza kila kitu na kuendelea na shughuli zako.
Aidha, Waziri Ummy ameitaka Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) iendeshe kliniki hiyo mpya ya wagonjwa maalum na wa kimataifa kwa ubia na wawekezaji wengine ili kuboresha zaidi huduma zitolewazo.

“Ni jambo zuri sana mmelianzisha lakini tusije kukwama njiani hivyo tushirikiane na wadau wengine ili huduma hii iendelee na ni matarajio yangu kwamba kliniki hii mpya ya wagonjwa maalumu na wagonjwa wa Kimataifa itakuwa kliniki ya mfano ambayo itakua kivutio kikubwa kwa wagonjwa kutoka katika Mataifa mbalimbali”. Amesema Waziri Ummy.

Amesema, Kutokana na uwekezaji mkubwa katika miundombinu vifaa tiba na wataalamu, Taasisi ya MOl imefanikiwa kupunguza rufaa za wagonjuwa kwenda nje ya nchi ambapo hivi sasa 99% ya huduma za mifupa zinapatikana hapa nchini na 97% ya huduma za kibingwa za Ubongo, Mgongo na Mishipa ya Gahamu zinapatikana hapa chini.

Naye Meneja Mkuu wa Vertex Group Experts Herbert Swai ameipongeza jitihada za Rais Samia Suluhu Hassan kwa kusikiliza kilio cha Watanzania na kuboreha huduma za Afya ikiwemo kutoa fedha kwaajili ya majengo, vifaa na vifaa tiba na Sasa tunakwenda kuwa kitovu cha Tiba Utalii.

“kampuni yetu itaendelea kuwa kinara katika kutoa huduma bora kwa wateja, tunawakaribisha watanzania wote na waafrika kushirikiana nasi, Kwa pamoja, tunaweza kutoa huduma nyingi zaidi, na kuhakikisha kwamba wateja wetu na washikadau wananufaika kutokana na wigo mpana wa masuluhisho yanayolenga mahitaji yao.” Alisema.

About the Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

You may also like these