HUDUMA YA AFYA MAJUMBANI VERTEX KUSAIDIA DIASPORA KUUGUZA

WATANZANIA waishio nje ya nchi maarufu kwa jina la Diaspora wametakiwa kutumia kampuni ya Vertex kwenye kusimamia afya na matibabu ya wazazi ndugu na jamaa zao. Akizunguma jijini Dar es Salaam katika mahojiano na waandishi wa habari, Meneja wa Kampuni ya Veltex, Herbert Swai amesema kwa kutumia kampuni hiyo Mtanzania aishie nje sasa wataweza kusimamia matibabu ya wazazi wake akiwa nje ya nchi kwa njia ya uhakika. Hofu kuu ya watanzania ya watanzania waishio nje ya nchi ni pale wanapopata mgonjwa nyumbani halafu wakashindwa kuwepo kuwasimamia wapendwa wao.


Sisi kama vertex tumeliona hilo; tumeingiza katika huduma zetu, usimamizi wa afya ya mgonjwa kuanzia nyumbani hadi hospitalini.
‘Mmoja ya huduma ambazo tunazitoa mbali na tiba utalii, ni huduma ya afya majumbani ambayo mgonjwa anasimamiwa na kampuni yetu kupata matibabu akiwa nyumbani, au anasimamiwa akiwa hospitalini chini ya mtoa huduma wetu.”amesema Herbart alisema wanaipendekeza huduma hii kwa watanzania washio nje ya nchi kwakuwa imeonyesha mafanikio makubwa na kurejesha Amani wa diaspora.


Amefafanua kuwa Vertex wanahakikisha wanasimamia kutaratibu mlolongo mzima wa huduma ya afya kama ndugu wa karibu wa mgonjwa.
Alisema wanasimamia kuanzia kusafirisha wagonjwa kutoka sehemu moja kwenda nyingine, kwa wagonjwa walio nje ya nchi kukata tiketi, kupata Viza ya kuja nchini kupokelewa akifika nchini hata kama mgonjwa anayekuja ni mahututi ataweza kupokelewa kwa njia ya usalama kwa ambulance maalum na maafisa kutoka ndani ya kampuni hiyo.
Alisema wanahakikisha wanasimamia malazi, kuandaa appointment ya kuonana na madaktari bobezi kwakusimamiwa na maafisa kutoka kampuni hiyo.
Amesema aina za huduma za afya za majumbani ambazo mgonjwa anaweza kupokea kutoka kwenye kampuni hii hazina kikomo. “Tunaangalia mahitaji kulingana na hali ya mgonjwa binafsi, huduma hizi zinaanzia kwenye kutibiwa na Daktari kwa njia ya simu uuguzi hadi huduma maalum za matibabu, kama vile kuchukua na kurudisha vipimo na majibu kutoka nyumbani hadi maabara.
“mgpnjwa na daktari wake wataamua mpango wao wa utunzaji na huduma ambazo unaweza kuhitaji nyumbani. Sisi tunaingia kukupatia Huduma hizo za ukiwa nyumbani.”
Herbet amesema huduma zao zimeenda mbale Zaidi ikiwa ni kumtafutia mgonjwa Daktari ambaye anaweza kumtembelea mgonjwa nyumbani ili kuchunguza na kutibu ugonjwa. Anaweza pia kukagua mara kwa mara mahitaji ya utunzaji wa afya yake akiwa nyumbani.
“Huduma ya afya ya nyumbani ya uuguzi hutolewa kulingana na mahitaji ya mtu. Kwa kushauriana na daktari, muuguzi aliyesajiliwa kutoka kwetu ataweka mpango wa namna ya kutoa huduma hizo. Huduma ya uuguzi inaweza kujumuisha kufunga jeraha, utunzaji wa ostomy, matibabu ya kuchua mishipa, kutoa dawa, ufuatiliaji wa afya ya jumla ya mgonjwa kama kupima presha na sukari, udhibiti wa maumivu, na usaidizi mwingine wa afya.” amesema
Amesema Wagonjwa wengine wanaweza kuhitaji usaidizi wa kujifunza upya jinsi ya kutekeleza majukumu ya kila siku mfano wagonjwa wa sukari ambao inabidi wajifunze kuchoma sindano kiusahihi. Mtaalamu wa tiba ya kimwili anaweza kuja nyumbani kwako kwa ajili ya kukuongoza katika safari ya kujihudumia.
Mtaalamu wa matibabu anaweza kumsaidia mgonjwa aliye na ulemavu wa kimwili, maendeleo, kijamii, au kihisia kujifunza upya jinsi ya kufanya kazi za kila siku kama vile kula, kuoga, kuvaa, na zaidi. Mtaalamu wa tiba ya usemi anaweza kumsaidia mgonjwa aliye na matatizo ya kuzungumza kurejesha uwezo wa kuwasiliana vizuri.
Wafanyakazi wetu wa matibabu wa kijamii hutoa huduma mbalimbali kwa mgonjwa, ikiwa ni pamoja na ushauri nasaha na kutafuta rasilimali za jamii ili kumsaidia mgonjwa katika kupona kwake.
Huduma nyinginezo ni wasimamizi wa kesi za mgonjwa– ikiwa hali ya matibabu ya mgonjwa ni ngumu sana na inahitaji uratibu wa huduma nyingi, washauri wanakuwa sehemu ya mkakati na usimamizi.

“Wasaidizi wa afya ya nyumbani wanaweza kumsaidia mgonjwa na mahitaji yake ya kimsingi ya kibinafsi kama vile kuamka kitandani, kutembea, kuoga, na kuvaa. Wasaidizi wetu wamepata mafunzo maalumu ili kusaidia uangalizi maalumu zaidi chini ya uangalizi wa muuguzi.” Alisema Herbart.
Amesema Mgonjwa anapohudumiwa nyumbani, mfanyakazi wa nyumbani au mtu anayemsaidia kazi anaweza kufaidia na maelekezo ya jinsi kuandaa chakula, na vitu vingine vya utunzaji wa mgonjwa, mtaalamu wetu akiwa hayupo.

About the Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

You may also like these