VERTEX YAADHIMISHA SIKU YA WANAWAKE NA WACHUUZI

Akizungumza jijini Dar es Salaam katika viwanja vya Mnazi Mmoja katika maadhimisho hayo ya Siku ya Wanawake Meneja wa Kampuni ya Vertex, Herbert Swai amesema vertex ni wadau wa matibabu ya Afya Nchini ambao kwa kutumia kampuni hiyo Mtanzania ataweza kutafutiwa matibabu kwa njia ya haraka hapa Nchi na hata kwenda nchi za nje kama Uturuki, Uingereza, India, Afrika Kusini na nchi zingine kupatiwa matibabu kwa haraka na uhakika.

Pia Vertex wanaitangaza Tanzania kwa kuwaalika wagonjwa kutoka nchi jirani kuja katika matibabu katika hospitali za Serikali ikiwemo Muhimbili na Jakaya Kikwete (JKCI) kuja kupata matibabu yao kwa haraka na uharaka na uhakika.

Amefafanua wanahakikisha wanasimamia utaratibu wa kukata tiketi, kupata Viza ya kuja nchini jinsi ya kuweza kupokelewa akifika nchini hata kama mgonjwa anayekuja ni mahututi ataweza kupokelewa kwa njia ya usalama kwa ambulance maalum na maafisa kutoka ndani ya kampuni hiyo.

Kuhakikisha wanasimamia malazi, kuandaa appointment ya kuonana na madaktari bobezi kwakusimamiwa na maafisa kutoka kampuni hiyo.

Amefafanua Vertex inaunga mkono juhudi za Rais Samia Suluhu Hassan katika kutangaza utalii tiba kuitangaza Tanzania kuwa kama kitovu cha matibabu ya afya na kutangaza madaktari wetu bingwa waliopo nchini.

“Tayari tumeshahudumia zaidi ya wagonjwa ya 68 katika huduma hizo kwa kuimarisha afya za watu” amefafanua

About the Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

You may also like these