Amesema Rais Dk. Samia katambulisha Tanzania katika Afrika Mashariki ni kitovu cha huduma bora za afya lazima wafanye kazi ya kutoa huduma bora kwa wagonjwa wa nje wanaokuja kutibiwa nchini.
Swai amesema kwa takwimu zao mwaka 2023 walipokea wagonjwa 47 kutoka nchi mbalimbali walitibiwa nchini katika Hospitali ya Muhimbili na Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI).
Aidha amesema kwa sasa wanakabiliwa na changamoto ya wagonjwa wanakuja kutibiwa wengine wanakuwa hawajui lugha, kiswahili wala kingereza wanaongea lugha zao hivyo wanawakalimani kwa ajili ya wagonjwa wa nje ya nchi.
Ameongeza kuwa tiba utalii inawahusu watanzania wote na wapo kwa ajili ya kuwahudumia na kuwasiidia kupata huduma kwa haraka na wapo kisheria wanatambulika.
Mmoja wa wagonjwa kutoka visiwa vya Comoro waliopata huduma ya kutibiwa kupitia kampuni hiyo, Mohamed Abdulla amesema wanaishukuru imewawezesha kupata huduma katika Hospitali ya Taifa Muhimbili na wanaendelea vizuri.
“Tunaahaidi kuwa mabalozi wazuri na kuwashauri wananchi wa Comoro kutibiwa Tanzania kwa sababu kuna huduma nzuri kama hauna ndugu wa kukusaidia kuna kampuni ambayo inasimamia kuanzia matibabu yako hadi mwisho,”amesema Abdulla.